Baraza la Seneti la Kenya linakutana kuanza kusikiliza hoja ya kuondolewa kwa Gachagua

Baraza la Seneti la Kenya linakutana kuanza kusikiliza hoja ya kuondolewa kwa Gachagua

Baraza la Seneti la Kenya linakutana kwa ajili ya kuanza kusikiliza hoja ya kuondolewa madarakani Naibu Rais Rigathi Gachagua. Hoja hiyo inamtuhumu Gachagua kwa ufisadi, ukaidi, kuidhoofisha serikali na kuendesha siasa za migawanyiko ya kikabila, miongoni mwa mashtaka mengi ambayo ameyakanusha vikali. Spika wa Baraza la Seneti, Amason Jeffah Kingi, amesema vikao vya kusikiliza hoja hiyo vimeanza saa tatu asubuhi kwa saa za Afrika Mashariki. Baraza hilo linatarajia kuwa na siku 10 kwa ajili ya kukamilisha kesi hiyo na kufanya uamuzi kuhusu hoja hiyo, ambayo itahitaji kuungwa mkono na takribani theluthi mbili ya maseneta ili kuidhinishwa. Iwapo ataondolewa, Gachagua atakuwa naibu rais wa kwanza kuondolewa madarakani kwa njia hiyo tangu hoja ya kuondolewa madarakani ilipoingizwa katika katiba ya Kenya iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2010.

Related Articles

Visitor Counter

000833
Today: 3
Yesterday: 6
This Week: 41
Last Week: 60
This Month: 165

Opening Hours

  • Monday: 8.30am–6.30pm
  • Tuesday: 10.00am–8.00pm
  • Wednesday: 8.30am–6.30pm
  • Thursday: 8.30am–7.00pm
  • Friday: 8.30am–3.00pm
  • Saturday: 8.30am–2.00pm
  • Sunday: 8.30am–2.00pm

Contact Us

Kanani A Road, Mumasama Street,

P.O.BOX, 137

Ngara, Tanzania

Mobile:  +255 744 172 741

Email: info@ishizwemedia.co.tz