Waliofia Kariakoo kuagwa leo

Waliofia Kariakoo kuagwa leo

Miili 13 ya watu waliopoteza maisha baada ya kudondokewa na jengo katika eneo la biashara la Kariakoo, wilayani Ilala jijini Dar es Salaam itaagwa leo Jumatatu Novemba 18 saa saba mchana.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuongoza ndugu, jamaa na marafiki katika hafla fupi ya kuaga miili hiyo iliyopangwa kufanyika katika viwanja vya mnazi mmoja.

Rais Samia Suluhu Hassan tayari ameelekeza uchunguzi wa kina ufanyike katika majengo yote ya Kariakoo ili kuchukua tahadhari mapema na kuepusha madhara ya majengo kuporomoka na kuua raia.

Zoezi la ukoaji linahitaji kutumia  akili zaidi  na sio nguvu - Chalamila.

Zoezi la ukoaji linahitaji kutumia akili zaidi na sio nguvu - Chalamila.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema zoezi la uokoaji kufuatia ajali ya kuporomoka kwa ghorofa katika eneo la Soko la Kimataifa la Kariakoo linaloendelea tangu kutokea kwa ajali hiyo linahitaji kutumia akili kubwa zaidi na sio nguvu kama ambavyo wengi wanataka.

Akizungumza na waandishi wa habari akiwa Kariakoo, Chalamila amewatoa hofu baadhi ya watu wanaona kama zoezi la uokoaji linaenda taratibu na kuwasihi wawe watulivu wakati vikosi vya uokoaji vikiendelea na zoezi hilo hadi hapo wataalamu watakaposema sasa jengo hilo linaweza kubomolewa.

Auawa kwa kunyweshwa Saruji

Auawa kwa kunyweshwa Saruji

Mwili wa mwanaume ambaye Jina lake halijafahamika umekutwa umeuawa vichakani ukiwa na jeraha usoni huku ikioneshwa kunyweshwa saruji.

Mwili wa mtu huyo umeonekana katika vichaka vya mlima wa Uledi kata ya mpela manispaa ya Tabora Novemba 16,2024 baada ya waponda kokoto wa eneo hilo kubaini kuwa Kuna mwili katika eneo hilo.

Mashuhuda wa tukio hilo Enock Msonde na Pili Issa wanaojishughulisha na uchimbaji wa mawe na kuponda kokoto wamesema mwili huo wameukuta ukiwa na saruji mdomoni na puani na kupata hisia kuwa mtu huyo aliuawa kwa kupigwa na kunyweshwa saruji.

Kamanda wa Polisi mkoani Tabora Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Richard Abwao amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo na amesema uchunguzi wa kubaini chanzo cha tukio hilo unaendelea utakapokamilika taarifa itatolewa huku akiwataka wananchi au ndugu kufika katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tabora – Kitete kwa ajili ya kutambua mwili huo.

 Tanzania na Marekani zajadili uwindaji wa kitalii kwa njia ya mtandao

Tanzania na Marekani zajadili uwindaji wa kitalii kwa njia ya mtandao

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Pindi Chana  amefanya mazungumzo kwa njia ya mtandao na ujumbe kutoka idara ya Uvuvi na Wanyamapori ya Serikali ya Marekani kujadili  pendekezo la taasisi zisizokuwa za kiserikali la kupinga kuingizwa Marekani nyara zinazotokana na uwindaji wa tembo katika vitalu vya uwindaji wa kitalii kwenye eneo la West Kilimanjaro linalopakana na Hifadhi ya Amboseli Nchini Kenya.

Kikao hicho kimefanyika katika Makao Makuu ya Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) jijini Arusha  Novemba 14,2024.

Ujumbe wa Marekani umeeleza kuwa vikundi vilivyopeleka pendekezo (petition) vinadai kuwa Tanzania inawinda tembo wa amboseli ambao wanafanyiwa utafiti, uwindaji huo unakiuka makubaliano ya  miaka 30 ya kusitisha uwindaji katika eneo la West kilimanyaro - Amboseli na unatishia kupotea kwa tembo wenye meno makubwa. 

Waziri kwa kushirikiana na jopo la wataalam wakiongozwa wa Dkt. Alexander Lobora  ametoa ufafanuzi kuhusu utaratibu wa uwindaji wa tembo, mchango wake katika uhifadhi na maendeleo ya jamii na kwamba uwindaji unafanyika kisheria kwa kuzingatia utafiti na uzoefu wa muda mrefu. 

Aidha, Wizara imekanusha tuhuma hizo na imeushauri uongozi wa US Fish & Wildlife Service kupuuzia pendekezo lililowasilshwa na vikundi hivyo.

TAWIRI  Yabainisha Benki za  Sampuli za Kibaiolojia Katika Maabara.

TAWIRI Yabainisha Benki za Sampuli za Kibaiolojia Katika Maabara.

Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) kupitia Sehemu ya Sayansi ya Tiba na Maabara ya Wanyamapori imebainisha benki za sampuli za kibaolojia katika maabara, zinazosaidia kupata taarifa za uchunguzi wa kisayansi zinazotumika katika uhifadhi endelevu wa wanyamapori hapa nchini .

Akizungumza wakati wa zoezi la kuchakata na kuhifadhi sampuli hizo na taarifa zake, mtaalam wa maabara kutoka TAWIRI Anselmi Munga amesema, TAWIRI inajivunia kuwa na maabara za wanyamapori katika vituo vya Utafiti wa Wanyamapori Serengeti, Nyanda za juu Kusini na Makao Makuu ya Taasisi ambapo ndani yake kuna sampuli za kibaolojia za aina mbalimbali za wanyamapori zenye zaidi ya miaka 30.

“Benki hizi ni muhimu kwani hutunza sampuli za Kigenetiki, seli za kisomatiki, tishu, damu, na kuwa na datakanzu ya kisayansi ya wanayamapori wakiwemo waliokatika hatari ya kutoweka” amebainisha Munga.

Aidha, Munga ameeleza TAWIRI imeweka mkakati katika uhifadhi na utunzaji wa sampuli na taarifa zake kwa kuwezesha maabara kuwa na mfumo mzuri wa nishati ya umeme ambapo kuna majokofu yanayotumia umeme wa jua naumeme wa dharura (generator).

Pia sampuli zinahifadhiwa kwa kutumia mitungi ya kimiminika cha Naitrojeni na kemikali Munga Ameeleza, sampuli za wanyamapori zinatumika kusaidia katika mashtaka ya kijangili (forensic), kuandaa msingi wa utambuzi wa vinasaba (DNA) pamoja na kutoa taarifa za mabadiliko ya wanyamapori (evolution)

“kwa kutumia sampuli hizi tunaweza kubaini changamoto zinazokabili aina fulani ya wanyamapori kama vile magonjwa hivyo kuongeza jitihada za kuzuia na kudhibiti magonjwa hayo ” ameeleza Munga

Visitor Counter

000833
Today: 3
Yesterday: 6
This Week: 41
Last Week: 60
This Month: 165

Opening Hours

  • Monday: 8.30am–6.30pm
  • Tuesday: 10.00am–8.00pm
  • Wednesday: 8.30am–6.30pm
  • Thursday: 8.30am–7.00pm
  • Friday: 8.30am–3.00pm
  • Saturday: 8.30am–2.00pm
  • Sunday: 8.30am–2.00pm

Contact Us

Kanani A Road, Mumasama Street,

P.O.BOX, 137

Ngara, Tanzania

Mobile:  +255 744 172 741

Email: info@ishizwemedia.co.tz