Ikiwa imebaki viti 20 pekee kuhesabiwa kati ya jumla ya 465, chama tawala cha Waziri Mkuu Shigeru Ushiba cha Liberal Democratic Party, LPD ambacho kimetawala Japan tangu kumalizika kwa vita vya pili vya Dunia, pamoja na chama shirika cha Kimeito vimechukua viti 209 kwenye Bunge dogo.
Idadi hiyo imeshuka kutoka viti vya bunge 279 vilivyo kuwa navyo awali, ikiashiria uchaguzi mbaya zaidi kwa chama hicho tangu 2009, pale kilipopoteza utawala wake kwa muda mfupi. Keiichi Ishii aliyechukua utawala wa chama cha Komeito mwezi uliopita pia alipoteza kiti chake kwenye uchaguzi huo.
Mshindi mkubwa kwenye uchaguzi huo ni chama cha upinzani cha Constitutional Democracy Party of Japan, CDPJ, ambacho kimepata viti 143 kufikia sasa kutoka 98 kilichukuwa nazo hapo awali, ikionekana kwamba wapiga kura wanaadhibu chama tawala kutokana na kashfa za kifedha pamoja na mfumuko wa bei za bidhaa.
Matokeo hayo huenda yakalazimisha vyama kuingia kwenye makubaliano ya miungano na kwa hivyo kuwa na uwezekano wa udhaifu wa kisiasa, wakati taifa hilo lilikabiliana na changamoto za kiuchumi, na kiusalama.