Wakati mataifa mengi yakijaribu kubashiri ushindi wa Trump utaathiri vipi sera za kigeni za Marekani, wachambuzi wanasema kuwa huenda Beijing inalenga kutenganisha Marekani na Umoja wa Ulaya.
Mtaalam wa sera za kigeni za China kwenye Baraza la Ulaya la Ushirikiano wa Kigeni Alicia Bachulska amesema kuwa Ulaya inafahamu vyema kuhusu athari za sera za kigeni na kiviwanda za China kwenye soko moja, pamoja na usalama wa NATO kwenye ukanda wa mashariki.
Wakati wa uzinduzi wa mtandao wa wataalam wa China kuhusu Ulaya, kwenye chuo Kikuu cha Masomo ya Kigeni mjini Beijing Novemba 9, naibu kiongozi wa Masuala ya Ulaya kwenye wizara ya mambo ya kigeni ya China, Cao Lei, alieleza ushindi wa Trump huenda ukabadili maneno na ni muhimu kwa China kumaliza migawanyiko na kuimarisha ushirikiano na mataifa mengine.