Daktari wa viungo Haruna Ayubu, maarufu kama Rubai, mwenye Umri wa Miaka 63 mkazi wa Bukoba, ametuhumiwa kumbaka mtoto wa miaka 12 katika kipindi cha kati ya Desemba 2023 na Oktoba 2024 ambapio kesi hiyo inasikilizwa katika Mahakama ya Wilaya ya Bukoba.
Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, Rubai alimvua nguo Mtoto huyo na kumwingilia kimwili mara kadhaa, kisha kumpatia fedha kwa ajili ya kuwapelekea Wazazi wake. Mnamo Oktoba 19, mtoto ambaye ni mhanga wa tukio hilo alikamatwa na askari Polisi baada ya kutoka ofisini kwa mshtakiwa na uchunguzi wa Daktari ulithibitisha kuwa Mtoto huyo alibakwa.
Upande wa mashtaka una mashahidi 10, vielelezo vya maandishi vitatu, na ripoti ya Daktari hata hivyo Wakili wa mshtakiwa, Frank John, aliiomba Mahakama kuahirisha kesi ili apate muda wa kuandaa utetezi na kuzungumza na mteja wake huku upande wa mashtaka ukiomba kesi hiyo kusikilizwa haraka kwa maslahi ya mtoto ili asiendelee kuja Mahakamani mara kwa mara.
aidha, Mahakama iliweka masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini wawili wenye mali zisizohamishika zenye thamani ya milioni nne kila mmoja ambapo kesi hiyo itatajwa tena Oktoba 29, 2024.