Droo ya Kombe la Shirikisho Afrika imepangwa muda mchache uliopita jijini Cairo Misri kwa ajili ya kuanza hatua ya Makundi msimu wa 2024/2025.
Simba SC ndio muwakilishi wa Tanzania ambapo amepangwa Kundi A na timu za CS Sfaxien ya Tunisia, CS Constantine ya Algeria na FC Bravos wa Angola.
Ikumbukwe kuwa kila Kundi timu mbili ndio zitafuzu kucheza robo fainali, kwenye Kundi la Simba kuna timu za kutoka Mataifa ya Afrika Kaskazini ambayo yana nguvu katika soka la Afrika vipi Simba atatoboa?