Siku nya jumapili Israel imesema kuwa imeanzisha uvamizi wa ardhini nchini Syria, kushikilia kile kilichoelezwa na Syria kujihusisha na mitandao ya Iran inayowasaidia wanamgambo katika eneo hilo.
Uvamizi wa Israel, nchini Syria, umekuwa wa kwanza katika kipindi cha miezi mitatu ya mgogoro wa mashariki ya kati. Syria haikujibu kwa haraka kuthibitisha madai ya oparesheni hiyo.
Jeshi la Israel halikusema sehemu ambapo uvamizi huo umefanyika , lakini limemtaja mtu liliye mshikilia kuwa ni Ali Soleiman al-Assi, na inaelezwa kuwa amekuwa akiishi katika mkoa wa kusini wa Syria, wa Saida.
Israel imesema alikuwa chini ya uchunguzi wa kijeshi kwa miezi kadhaa, na alijihusisha katika juhudi za Iran, na kulenga maeneo ya Israel yenye mgogoro ya milima ya Golani karibu na mpaka wa Syria.