Jamii yashauriwa kuzingatia taratibu na kanuni za lishe bora.

Jamii yashauriwa kuzingatia taratibu na kanuni za lishe bora.

Wananchi wilaya Ngara mkoani Kagera wameshauriwa kuzingatia taratibu na kanuni za lishe bora kwa ajili ya kuboresha afya zao na kujikinga dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza.

Hayo yamesemwa na katibu tawala wilaya Ngara Bi. Hatujuani Ally Lukari kwa niaba ya mkuu wa wilaya hiyo Col. Mathias Kahabi wakati wa hafla ya uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya lishe uliofanyika katika uwanja wa kokoto mjini Ngara. Bi. Hatujuani ameeleza kuwa lishe sio kujaza tumbo bali ni kuzingatia miongozo ya mlo kamili hususani aina sita za makundi ya chkula.

Kwa upande wake Afisa lishe wilaya ya Ngara Emmanuel Msokwa amesema ili jamii iweze kukua katika misingi iliyo bora, uzingatiaji wa lishe ni jambo muhimu sana hivyo wananchi hawana budi kuzingatia makundi sita ya chakula ambayo ni vvakula vya nafaka na mizizi, vyakula jamii ya kunde, wanyama na mazao yake, mbogamboga, matunda na mafuta ambayo yanayohitajika kwa kiwango kidogo.

Related Articles

Visitor Counter

000833
Today: 3
Yesterday: 6
This Week: 41
Last Week: 60
This Month: 165

Opening Hours

  • Monday: 8.30am–6.30pm
  • Tuesday: 10.00am–8.00pm
  • Wednesday: 8.30am–6.30pm
  • Thursday: 8.30am–7.00pm
  • Friday: 8.30am–3.00pm
  • Saturday: 8.30am–2.00pm
  • Sunday: 8.30am–2.00pm

Contact Us

Kanani A Road, Mumasama Street,

P.O.BOX, 137

Ngara, Tanzania

Mobile:  +255 744 172 741

Email: info@ishizwemedia.co.tz