Bunge la Seneti nchini Kenya limeanza rasmi hatua ya mwisho ya kumuondoa madarakani Naibu Rais Rigathi Gachagua.
Wiki iliyopita wabunge walipiga kura katika Bunge la Kitaifa kuidhinisha kuondolewa kwake madarakani na hivyo kuweka mazingira ya kusikilizwa kwa kesi ya siku mbili katika Seneti ambayo itaamua iwapo atamtimua au la.
Naibu Rais anakabiliwa na mashtaka 11 yakiwemo ufisadi, kuchochea migawanyiko ya kikabila na kuhujumu serikali ingawa Naibu huyo anakanusha madai hayo.
Mchakato huo unafuatia mzozo wake wa hivi majuzi na Rais William Ruto, ambaye amekuwa kimya kuhusu suala hilo.