Waasi wa M23 wamekubaliana na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC, juu ya kuondoka kwa vikosi vyake kutoka mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ikiwa ni siku chache baada ya wakuu wa majeshi wa Afrika Kusini, Zambia, Malawi na Tanzania kukutana na mkuu wa jeshi la M23 Sultani Makenga katika mji wa Goma.
Pande zote mbili zimekubaliana, kwamba M23 itawezesha kuondoka mara moja kwa askari wa kikosi hicho kupitia uwanja wa ndege wa Goma, ambao kwa sasa hautumiki kwa sababu ya kuharibiwa wakati wa mapigano.