Serikali inataka rudisho la uwekezaji ‘return on investment’ katika kampuni ambazo serikali inaumiliki wa hisa chache kuongezeka kutoka asilimia saba ya sasa hadi kufikia zaidi ya asilimia 10 katika mwaka ujao wa fedha
Dhamira hiyo ilielezwa Machi 28, 2025, na Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Moses Kusiluka wilayani Kibaha, mkoani Pwani, wakati wa kufunga mkutano wa siku tatu wa wakurugenzi wa bodi za kampuni ambazo serikali inaumiliki wa hisa chache.
“Niwape changamoto ya kukuza rudisho la uwekezaji kutoka asilimia saba ya sasa kwenda zaidi ya asilimia 10 kwa mwaka ili kufikia azma hii mnapaswa kuongeza ufanisi wa utendaji," alisema.
alisema Ofisi ya Msajili wa Hazina inasimamia jumla ya taasisi 308 ambapo kati ya hizo 56 ni zile ambazo serikali ina umiliki wa hisa chache, jumla ya uwekezaji wa Shlilingi trilioni 86.3, umefanywa katika taasisi hizo, huku kati ya kiasi hicho Shilingi trilioni 2.9 trilioni zikiwekezwa kwenye kampuni ambazo serikali ina umiliki wa hisa chache na Shilingi trilioni 83.4 ikienda kwa taasisi ambazo serikali ina umiliki wa asilimia 100.
Aidha, Balozi Kusiluka aliwapa changamoto wakurugenzi wa bodi za kampuni ambazo ina hisa chache kuongeza ufanisi gawio kwa serikali.