Madaktari wa macho katika hospitali ya Rufaa ya mkoa Kagera (Bukoba) kwa kushirikiana na kituo cha Tumaini Children Centre, wameendesha zoezi la upimaji wa macho kwa watoto waishio mitaani wapatao 24. Kupitia zoezi hilo, Daktari Bingwa wa Macho wa hospitali ya Rufaa ya mkoa Kagera, (Bukoba) Dr. Daniel Mashamba alitoa elimu ya afya ya macho kwa watoto hao huku akiwashauri kujiepusha na michezo hatarishi inayoweza kuathiri macho yao.
"Tumeona baadhi yenu macho yenu yako sawa lakini wengine macho yenu yana matatizo, tumeongea na wenzetu wa kituo cha Tumaini Children Centre watawaleta wale waliogundulika kuwa na matatizo ili mpatiwe dawa lakini mmoja wenu anatakiwa kupatiwa miwani hivyo tutampatia, ninawashauri tunzeni macho yenu msicheze michezo hatarishi inayoweza kusababisha matatizo ya macho " alisema Dr. Mashamba.
Kwa upande wake mshauri wa kituo cha Tumaini Children Centre, Jovith Paschale ametoa shukrani zake kwa viongozi, madaktari na wataalam wa hospitali ya Rufaa ya mkoa Kagera, (Bukoba) kwa kushiriki katika maadhimisho ya Wiki ya Uoni Duniani kwa kutoa huduma za vipimo na elimu ya macho bure kwa watoto