Mjumbe wa Umoja wa Mataifa wa Sahara Magharibi, Staffan de Mistura ametoa wazo la kugawanywa kwa eneo hilo kati ya Morocco na Polisario Front, kama hatua ya kumaliza mzozo uliodumu kwa karibu miongo mitano
Mzozo huo ulioanza 1975 ni kati ya Morocco inayoitazama Western Sahara kama himaya yake na kundi la Polisario Front, linaloungwa mkono na Algeria, likiitisha kujitawala. kwa upande wa inchi ya Morocco inasema kuwa inaweza tu kuruhusu eneo hilo kujitawala likiwa chini ya serikali yake, lakini Polisario Front limekuwa likiitisha kuwe na kura ya maoni kuelekea kujitawala kama nchi huru.
Wakati akizungumza faraghani mbele ya Baraza la Usalama la UN, de Mistura ambaye ni mwanadiplomasia wa siku nyingi kutoka Italy alisema kuwa ugawanyaji huo utaruhusu kubuniwa kwa taifa huru upande wa kusini na kwa upande mwingine kuruhusu Morocco kuchukua sehemu iliyobaki ikitambuliwa kimataifa.
Aliongeza kusema kuwa licha ya pendekezo hilo, pande zote mbili (Morocco na Polisario Front) hawakuridhia huku akisema kuwa Katibu Mkuu wa UN anahitaji kutathmini tena jukumu lake kama mjumbe maalum iwapo hakuna hatua zitakazokuwa zimepigwa kuelekea suluhisho la mzozo huo ndani ya miezi 6.