Mkandarasi Buzubona &Sons Co. Ltd ametambulishwa rasmi kwa mkuu wa wilaya ya Ngara Col Mathias Julius Kahabi kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa Mradi wa maji Kigina na Kumuyange kwa gharama ya shilingi za kitanzania bilioni 1.6
Mradi huu unatekelezwa kwa muda wa miezi 6 na unatakiwa kukamilika tarehe 10/03/2025 huku shughuli zitakazotekelezwa kwa upande wa Kumuyange ni ujenzi wa chanzo, tenki la Lita 25,000, tenki la Lita 75,000, mtandao wa bomba kilomita 10.8 na maunganisho ya majumbani kwa Kaya 50.
Kwa upande wa Kigina, Shughuli zitakazotekelezwa ni pamoja na ujenzi wa chanzo, tenki Lita 25,000, tenki Lita 50,000, tenki Lita 120,000, nyumba ya mitambo na ufungaji pampu ya Sola, vituo vya kuchotea maji 9, mtandao wa Bomba kilomita 26.6 na maunganisho ya maji majumbani kwa Kaya 100.