Paul Pogba amedhamiria kurejea kwenye soka kufuatia kupigwa marufuku kujihusisha na mchezo huo baada ya kupatikana na hatia ya kutumia dawa za kusisimua misuli .
Nyota huyo wa Juventus alifungiwa kwa miaka minne mwezi Februari baada ya kusimamishwa kwa muda na mahakama ya kitaifa ya Italia ya kupambana na dawa za kusisimua misuli (NADO Italia) Septemba mwaka jana.
Kufuatia kupigwa marufuku kwa muda, NADO Italia ilisema kuwa testosterone, ambayo inaweza kutumika kuongeza uvumilivu wa riadha, iligunduliwa kwenye mfumo wa kiungo huyo baada ya Juventus kuichapa Udinese 3-0, huku Pogba akiwa kwenye benchi kama mchezaji wa akiba ambaye hakutumika.
Akizungumza na Sky Sports kiungo huyo alisem,a kuwa watu walifahamu, na walipoona jambo hilo limetokea, walijua haikuwa makusudi “Mimi sio tapeli, mimi ni mtu ninayependa mchezo wangu na kupenda mchezo huo. Sipendi kudanganya, napenda kushinda kwa haki. Watu wanajua hilo. Mimi ni mpotevu mbaya lakini mimi si tapeli.” alisema kiungo huyo.
Pogba alifungiwa kucheza soka kwa miaka minne baada ya kukutwa na hatia ya kutumia dawa iliyopigwa marufuku ya testosterone iliyogunduliwa kwenye mwili wake, hata hivyo adhabu hiyo ilipunguzwa hadi miezi 18 na Mahakama ya Usuluhishi wa michezo ambapio nyota huyo anatarajia kurudi dimbani tena ifikapo Machi 2025.