Tanzania na Marekani zajadili uwindaji wa kitalii kwa njia ya mtandao

Tanzania na Marekani zajadili uwindaji wa kitalii kwa njia ya mtandao

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Pindi Chana  amefanya mazungumzo kwa njia ya mtandao na ujumbe kutoka idara ya Uvuvi na Wanyamapori ya Serikali ya Marekani kujadili  pendekezo la taasisi zisizokuwa za kiserikali la kupinga kuingizwa Marekani nyara zinazotokana na uwindaji wa tembo katika vitalu vya uwindaji wa kitalii kwenye eneo la West Kilimanjaro linalopakana na Hifadhi ya Amboseli Nchini Kenya.

Kikao hicho kimefanyika katika Makao Makuu ya Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) jijini Arusha  Novemba 14,2024.

Ujumbe wa Marekani umeeleza kuwa vikundi vilivyopeleka pendekezo (petition) vinadai kuwa Tanzania inawinda tembo wa amboseli ambao wanafanyiwa utafiti, uwindaji huo unakiuka makubaliano ya  miaka 30 ya kusitisha uwindaji katika eneo la West kilimanyaro - Amboseli na unatishia kupotea kwa tembo wenye meno makubwa. 

Waziri kwa kushirikiana na jopo la wataalam wakiongozwa wa Dkt. Alexander Lobora  ametoa ufafanuzi kuhusu utaratibu wa uwindaji wa tembo, mchango wake katika uhifadhi na maendeleo ya jamii na kwamba uwindaji unafanyika kisheria kwa kuzingatia utafiti na uzoefu wa muda mrefu. 

Aidha, Wizara imekanusha tuhuma hizo na imeushauri uongozi wa US Fish & Wildlife Service kupuuzia pendekezo lililowasilshwa na vikundi hivyo.

Related Articles

Visitor Counter

000833
Today: 3
Yesterday: 6
This Week: 41
Last Week: 60
This Month: 165

Opening Hours

  • Monday: 8.30am–6.30pm
  • Tuesday: 10.00am–8.00pm
  • Wednesday: 8.30am–6.30pm
  • Thursday: 8.30am–7.00pm
  • Friday: 8.30am–3.00pm
  • Saturday: 8.30am–2.00pm
  • Sunday: 8.30am–2.00pm

Contact Us

Kanani A Road, Mumasama Street,

P.O.BOX, 137

Ngara, Tanzania

Mobile:  +255 744 172 741

Email: info@ishizwemedia.co.tz