Maafisa wa Ujerumani wameendele kufanya msako mkali kwenye majimbo sita unaowalenga washukiwa 17 wanaotuhumiwa kuwa wanachama wa kundi la ndani la kigaidi linalolenga kuiangusha serikali ya Eritrea.
Waendesha mashitaka wa Ujerumani wamesema washukiwa hao wanaaminika kushikilia nyadhifa kubwa katika kundi la Brigade N'Hamedu - tawi la Ujerumani, ambalo limekuwa likiendesha harakati zake tangu mwaka 2022.
Kundi hilo linaelezwa kuwa mtandao wa kimataifa na linajulikana kwa kutumia vurugu dhidi ya wafuasi wa serikali ya Eritrea. Linatuhumiwa kwa kupanga ghasia katika matamasha ya Kieritrea mjini Giessen, karibu na Frankfurt Agosti 2022 na Agosti 2023, Pia kwenye warsha iliyoandaliwa na chama cha Kieritrea mjini Stuttgart mnamo Septemba 2023 huku takribani makazi 19 yamepekuliwa mapema leo nchini Ujerumani ambapo hadi sasa hakuna aliyekamatwa.