Vifo vilivyotokana na tetemeko la ardhi lililoikumba miji mbalimbali nchini Myanmar imefikia watu 1,000 huku mamia wengine wakihofiwa kunaswa kwenye vifusi vya majengo yaliyoanguka.
Mbali ya idadi hiyo ya vifo pia serikali ya nchi hiyo imesema kuwa idadi ya majeruhi ni zaidi ya watu 2,300 huku shughuli za uokoakji na kutafuta miili ya watu waliofariki na kufukiwa na vifusi ikiendelea kufanyika.
Miili 12 ya watoto wa chekechea na mwalimu wa shule ya Mye Mye Kyi imepatikana mapema leo kwenye eneo la Kyaukse lililopo kwenye mji wa Mandalay.
Viongozi wa kijeshi wa Myanmar wametoa ombi la msaada wa kimataifa huku China na India yakiwa amataifa ya awali kutoa msaada kwenye taifa hilo.
