Wapiga kura nchini Gabon wameidhinisha kwa wingi katiba mpya, ikiwa ni zaidi ya mwaka mmoja baada ya wanajeshi walioasi kumpindua rais wa muda mrefu wa nchi hiyo na kuchukua mamlaka katika taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa mafuta la Afrika ya Kati.
Katika taarifa yake Waziri wa Mambo ya Ndani wa Gabon Hermann Immongault iliyosomwa kwenye televisheni ya Taifa ilisema zaidi ya asilimia 91 ya wapiga kura wameidhinisha katiba mpya katika kura ya maoni iliyofanyika Jumamosi,
Aidha taarifa hiyo iliongeza kuwa watu waliojitokeza walikadiriwa kuwa asilimia 53.5 huku matokeo ya mwisho yakitarajiwa kutangazwa na Mahakama ya Katiba ya nchi hiyo.