Wamachinga Iringa watakiwa kukomesha migogoro

Wamachinga Iringa watakiwa kukomesha migogoro

Shirikisho la Umoja wa Machinga Tanzania (SHIUMA) limewataka wafanyabiashara wadogo maarufu kama machinga mjini Iringa kukomesha migogoro inayowagawa ili wawe na sauti moja katika kushughulikia masuala yao.

Wito huu umetolewa leo, na Katibu Mkuu wa SHIUMA Taifa, Venatus Magayane katika kongamano lililofanyika katika ukumbi wa Highlands Hall, Manispaa ya Iringa.

Katika kongamano hilo, Magayane alikiri kuwepo kwa tofauti kati yake na Naibu Katibu Mkuu wa SHIUMA Taifa, Joseph Mwanakijiji, ambaye pia alikuwa kiongozi wa Machinga Iringa. Alieleza kuwa baada ya majadiliano ya kina, wamekubaliana kumaliza tofauti zao na kufuta kesi zote zilizokuwa mahakamani kati yao.

Aidha , Mwanakijiji alisisitiza umuhimu wa umoja miongoni mwa machinga wa Iringa, akieleza kuwa ni muhimu kujitahidi pamoja ili kunufaika na fursa nyingi na mipango ya serikali inayowalenga.

Related Articles

Visitor Counter

000833
Today: 3
Yesterday: 6
This Week: 41
Last Week: 60
This Month: 165

Opening Hours

  • Monday: 8.30am–6.30pm
  • Tuesday: 10.00am–8.00pm
  • Wednesday: 8.30am–6.30pm
  • Thursday: 8.30am–7.00pm
  • Friday: 8.30am–3.00pm
  • Saturday: 8.30am–2.00pm
  • Sunday: 8.30am–2.00pm

Contact Us

Kanani A Road, Mumasama Street,

P.O.BOX, 137

Ngara, Tanzania

Mobile:  +255 744 172 741

Email: info@ishizwemedia.co.tz