Waziri wa Zamani wa Sheria Nchini Kenya, Martha Karua Afukuzwa Tanzania

Waziri wa Zamani wa Sheria Nchini Kenya, Martha Karua Afukuzwa Tanzania

Mwanasiasa aliyewahi kugombea urais wa Kenya, Martha Karua, ametimuliwa  nchini Tanzania na kurejehswa kwao baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam ambako alitaka kufuatilia kesi ya kiongozi wa Chama cha Demkrasia na Maendeleo (CHADEMA)  Tundu Lissu.

Wakili na mgombea Urais wa zamani nchini KenyaMartha Karua, amesema amefukuzwa kutoka nchini Tanzania ambako alipanga kuhudHuria kusikilizwa kwa kesi dhidi ya mwanasiasa mashuhuri wa upinzani anayekabiliwa na mashitka ya uhaini.

Karua, waziri wa zamani wa sheria wa Kenya, ambaye amekuwa msitari wa mbele kupiga kelele kuhusu kurudi nyuma kwa demokrasia Afrika Mashariki, kufukuzwa kwake ni ishara kwamba mamlaka za Tanzania hawataisikiliza kesi na kutoa hukumu ya haki kwa kiongozi wa upinzani wa chama cha Chadema Tundu Lissu.

Karua alisafiri kwenda Dar es Salaam kushuhudia na kufuatilia kesi ya Lissu ambaye anatarajiwa kupandishwa kizimbani leo Mei, 18, 2025  kwa mashitaka ya uhaini ambayo hukumu yake inaweza kuwa na adhabu ya kifo.

Karua alisema yeye na kundi lake walizuiwa walipowasili uwanja wa ndege wa Dar es Salaam na kutiwa kwenye ndege kurudishwa Kenya siku hiyo hiyo.

Related Articles

Visitor Counter

000727
Today: 8
Yesterday: 4
This Week: 8
Last Week: 91
This Month: 210

Opening Hours

  • Monday: 8.30am–6.30pm
  • Tuesday: 10.00am–8.00pm
  • Wednesday: 8.30am–6.30pm
  • Thursday: 8.30am–7.00pm
  • Friday: 8.30am–3.00pm
  • Saturday: 8.30am–2.00pm
  • Sunday: 8.30am–2.00pm

Contact Us

Kanani A Road, Mumasama Street,

P.O.BOX, 137

Ngara, Tanzania

Mobile:  +255 744 172 741

Email: info@ishizwemedia.co.tz