Miamba ya soka Tanzania Simba na Yanga, imetajwa kuwania kipengele cha Klabu bora ya mwaka katika tuzo za shirikisho la soka barani Afrika (CAF), zitakazotolewa Disemba 16 mwaka huu nchini Morroco.
Tuzo hizo zinazotarajiwa kutolewa Disemba 16 mwaka huu, katika jiji la Marrakech Morroco, Klabu za Simba na Yanga zitachuana na Al Ahly, Mamelodi Sundows, Tp Mazembe, Petro Atletico, Zamalek, RS Berkane, Dream FC na Esperance de Tunis katika kipengele cha Klabu bora ya mwaka.
Yanga na Simba zilifanikiwa kufika hatua ya robo fainali katika michuano ya klabu bingwa msimu uliopita, ambapo Klabu ya Yanga ilitolewa na Mabingwa wa Afrika kusini Mamelodi Sundows, wakati wekundu wa msimbazi waking’olewa na Mabingwa Al Ahly.
Kipengele kingine kilichotajwa ni mlinda lango bora wa mwaka ambapo golikipa wa Yanga Djigui Diarra anachauana vikali pamoja na golikipa wa Mamelodi Sundows Ronwen Williams, Andre Onana wa Manchester United na nyota wengine.