Wapandikizwa Ini baada ya kula uyoga wenye sumu -Ujerumani.

Wapandikizwa Ini baada ya kula uyoga wenye sumu -Ujerumani.

Mwanamume mmoja nchini Ujerumani na watoto wawili wamelazimika kupandikizwa ini katika hospitali ya Chuo Kikuu katika mji wa magharibi mwa Ujerumani wa Essen, baada ya kula uyoga wenye sumu. Kwa mujibu wa taarifa kutoka hospitali hiyo mgonjwa wa nne, ambaye ni mvulana mdogo wa miaka mitano alipata nafuu bila kupandikizwa ini.

Wote wanne, mmoja wao akiwa ni baba wa mmoja wa watoto hao, wamekuwa katika uangalizi wa wagonjwa mahututi katika hospitali hiyo tangu siku ya Jumanne ambapo walilazwa hospitalini wakiwa na hali mbaya huku wawili wakifanyiwa upasuaji wa kupandikizwa ini muda mfupi baada ya kufikishwa hospitali na mtoto mmoja alifanyiwa upasuaji huo baadaye.

Hadi hvi sasa hali za wagonjwa wote zinaendelea vizuri na wanafuatiliwa kwa karibu na kwa umakini.

Mapigano mapya yazuka Mashariki mwa DRC.

Mapigano mapya yazuka Mashariki mwa DRC.

Mapigano yamezuka kati ya waasi wa M23 na wanamgambo wanaoungwa mkono na serikali mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Mapigano hayo mapya yalivunja makubaliano ya usitishwaji mapigano ambayo yalikuwa yamedumu kwa wiki kadhaa.

Duru za eneo hilo zimeeleza kuwa alfajiri ya jana Jumapili, waasi wa M23 walipambana na wanamgambo wakizalendo na kuwajeruhi raia 14 wakiwemo vijana wawili. Usitishaji mapigano kati ya jeshi la DRC na waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda ulianza mapema mwezi Agosti kufuatia upatanishi wa Angola.

Mazungumzo ya amani kati ya Kinshasa na Kigali yalikwama, lakini duru mpya ya mazungumzo imepangwa kufanyika mjini Luanda mwishoni mwa wiki ijayo. Rwanda inadai kuwa kuwepo kwa kundi la Wahutu wenye msimamo mkali wa FDLR eneo hilo, ni tishio kwa usalama wake.

Tangu M23 ilipoanzisha tena mashambulizi mwishoni mwa mwaka 2021, wameteka maeneo makubwa ya eneo hilo la mashariki mwa Kongo lenye utajiri wa madini.

Mahakama yasitisha kuondolewa kwa Gachagua Madarakani.

Mahakama yasitisha kuondolewa kwa Gachagua Madarakani.

Mahakama kuu imesitisha utekelezwaji wa azimio la Seneti la kuidhinisha mashtaka ya kumuondoa madarakani Rigathi Gachagua uamuzi huo umetolewa muda mfupi tu baada ya Bunge la Kenya kuafiki uteuzi wa Kithure Kindiki kuwa Naibu wa Rais baada ya Rais William Ruto kuwasilisha jina lake kwenye bunge hilo.

Hapo jana Maseneta nchini humo waliidhinisha mashtaka 5 kati ya 11 dhidi ya Gachagua na kumuondoa ofisini, Gachagua alikosa kufika mbele ya maseneta kujitetea baada ya mawakili wake kusema alipatwa na maumivu makali ya kifua na kulazimika kulazwa hospitalini.

Uamuzi uliotolewa na Jaji E.C. Mwita umezuia kutekelezwa kwa azimio hilo la Seneti na pia kuzuia Rais kumteua mtu kuichukua nafasi hiyo hadi tarehe 24 mwezi huu kesi hiyo itakapo sikilizwa na jopo la majaji watakaoteuliwa na Jaji Mkuu Martha Koome. Hata hivyo tayari Rais amependekeza jina la Kithure Kindiki kuchukua nafasi ya Gachagua na bunge la taifa kuafiki uteuzi wake.

Mjumbe wa UN apendekeza Sahara Magharibi kupewa uhuru wake.

Mjumbe wa UN apendekeza Sahara Magharibi kupewa uhuru wake.

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa wa Sahara Magharibi, Staffan de Mistura ametoa wazo la kugawanywa kwa eneo hilo kati ya Morocco na Polisario Front, kama hatua ya kumaliza mzozo uliodumu kwa karibu miongo mitano

Mzozo huo ulioanza 1975 ni kati ya Morocco inayoitazama Western Sahara kama himaya yake na kundi la Polisario Front, linaloungwa mkono na Algeria, likiitisha kujitawala.  kwa upande wa inchi ya  Morocco  inasema kuwa inaweza tu kuruhusu eneo hilo kujitawala likiwa chini ya serikali yake, lakini Polisario Front limekuwa likiitisha kuwe na kura ya maoni kuelekea kujitawala kama nchi huru.

Wakati akizungumza faraghani mbele ya Baraza la Usalama la UN, de Mistura ambaye ni mwanadiplomasia wa siku nyingi kutoka Italy alisema kuwa ugawanyaji huo utaruhusu kubuniwa kwa taifa huru upande wa kusini  na kwa upande mwingine kuruhusu Morocco kuchukua sehemu iliyobaki ikitambuliwa kimataifa.

Aliongeza kusema kuwa licha ya pendekezo hilo, pande zote mbili (Morocco na Polisario Front) hawakuridhia huku akisema kuwa Katibu Mkuu wa UN anahitaji kutathmini tena jukumu lake kama mjumbe maalum iwapo hakuna hatua zitakazokuwa zimepigwa kuelekea suluhisho la mzozo huo ndani ya miezi 6.

Kesi ya kumuondoa Naibu Rais wa Kenya  kusikilizwa na Seneti

Kesi ya kumuondoa Naibu Rais wa Kenya kusikilizwa na Seneti

Bunge la Seneti nchini Kenya limeanza  rasmi hatua ya mwisho ya kumuondoa madarakani Naibu Rais Rigathi Gachagua.

Wiki iliyopita wabunge walipiga kura katika Bunge la Kitaifa kuidhinisha kuondolewa kwake madarakani na hivyo kuweka mazingira ya kusikilizwa kwa kesi ya siku mbili katika Seneti ambayo itaamua iwapo atamtimua au la.

Naibu Rais anakabiliwa na mashtaka 11 yakiwemo ufisadi, kuchochea migawanyiko ya kikabila na kuhujumu serikali   ingawa Naibu huyo     anakanusha madai hayo. 

Mchakato huo unafuatia mzozo wake wa hivi majuzi na Rais William Ruto, ambaye amekuwa kimya kuhusu suala hilo.

Visitor Counter

000833
Today: 3
Yesterday: 6
This Week: 41
Last Week: 60
This Month: 165

Opening Hours

  • Monday: 8.30am–6.30pm
  • Tuesday: 10.00am–8.00pm
  • Wednesday: 8.30am–6.30pm
  • Thursday: 8.30am–7.00pm
  • Friday: 8.30am–3.00pm
  • Saturday: 8.30am–2.00pm
  • Sunday: 8.30am–2.00pm

Contact Us

Kanani A Road, Mumasama Street,

P.O.BOX, 137

Ngara, Tanzania

Mobile:  +255 744 172 741

Email: info@ishizwemedia.co.tz