Mkuu wa wa wilaya ya Mbeya Beno Malisa kwa kushirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu TFS nyanda za juu kusini wamepanda miti Katika Shule ya Sekondari ya wasichana Loleza ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya kumbukizi ya miaka 25 ya kifo cha Rais wa kwanza na Baba wa Taifa la Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Zoezi hilo la upandaji miti limefanyika Katika Shule ya sekondari ya wasichana Loleza iliyopo jijini Mbeya ambapo mkuu wa wilaya hiyo ,ameambatana na Mhifadhi mkuu wa TFS Innocent Lupembe pamoja na Anamery Joseph mkuu wa kitengo cha maliasili na uhifadhi wa mazingira halmashauri ya jiji la Mbeya ambapo wamewaomba watanzania kutunza mazingira kwa kupanda miti ikiwa ni sehemu ya kumuenzi Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere.
Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi katika shule hiyo wametoa shukrani zao kwa wageni hao huku wakiahidi kuitunza miti hiyo na kuwa mabalozi wazuri wa mazingira kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho . Ikumbukwe kuwa, moja ya kauli za Mwalimu Nyerere kuhusu mazingira ni kuwa tunapokata miti bila kupanda ni deni haramu kwa sababu tunawahujumu wale ambao hawajazaliwa akiwa na lengo la kusisitiza watu kutunza mazingira kwa kupanda miti.