Israel yatangaza operesheni ya ardhini kusini magharibi mwa Lebanon

Israel yatangaza operesheni ya ardhini kusini magharibi mwa Lebanon

Jeshi la Israel lilitangaza Jumanne kuwa lilianzisha operesheni za ardhini kusini magharibi mwa Lebanon, kuashiria upanuzi wa uvamizi wake ambao maafisa wa Israel wamesema unalenga kuwarudisha nyuma wanamgambo wa Hezbollah kutoka mpakani.

Kama ilivyokuwa kwa operesheni zake za awali za ardhini nchini Lebanon zilizoanza Septemba 30, jeshi la Israeli lilielezea juhudi hizo mpya kama “operesheni ndogo, za ndani, zilizolengwa.” Kampeni hiyo ya ardhini inaambatana na mashambulizi makubwa ya angani, ambayo yamejumuisha mashambulizi ya anga kwenye mji mkuu wa Lebanon, Beirut, pamoja na maeneo ya kusini na mashariki mwa Lebanon.

Jeshi la Israel lilisema Jumanne moja ya mashambulizi hayo ya anga yalimuua kamanda mkuu wa Hezbollah, Suhail Husseini, ambaye alihusika katika uhamisho wa silaha kutoka Iran hadi kwa kundi la wanamgambo lenye makao yake nchini Lebanon.

Mwinyi “Tutashirikiana na sekta binafsi kufikia malengo ya afya”

Mwinyi “Tutashirikiana na sekta binafsi kufikia malengo ya afya”

Rais wa Zanzibar Dk Hussein Mwinyi amesema wanahitaji kuimarisha ushirikiano sekta binafsi na washirika wa maendeleo ili kufikia malengo ya afya bora kwa wananchi wote na kuondosha changamoto zinazoikabili sekta hiyo.

Changamoto hizo ni kupunguza vifo vya mama na mtoto, upatikanaji wa dawa muhimu, uimarishaji wa miundombinu ya afya, upatikanaji wa taarifa za afya, udhibiti wa maradhi ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza na mengineyo.

Rais Mwinyi ametoa kauli hiyo leo Oktoba 3, 2024 wakati akifunga kongamano la 11 la Tanzania Health Summitt (THS) lililofanyika katika Ukumbi wa Zanzibar International Trade Fair Fumba Nyamanzi Unguja.

“Tunahitaji kuendelea kuimarisha ushirikiano wa karibu na mashirika ya kimataifa na washirika wa maendeleo, kwani tumeona jinsi inavyofanikisha utekelezaji wa miradi mikubwa na kuimarisha mifumo ya afya nchini,” amesema Dk Mwinyi

Amesema wameshuhudia mifano mbalimbali ya jinsi ubia huo unavyoweza kuleta matokeo chanya katika upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wananchi hasa huduma za afya katika ngazi ya kati.

Amesisitiza kuwa changamoto zote zilizojadiliwa zinahitaji kuchukuliwa hatua madhubuti na za haraka.

Amesema tathmini ya mkutano huu imeonesha mafanikio makubwa yaliyopatikana katika sekta ya afya kupitia ubunifu na matumizi ya teknolojia, kama vile programu za afya za kidigitali zinazosaidia kuimarisha huduma za afya na mifumo ya taarifa za afya.

 

Waziri wa Afya Zanzibar, Ahmed Mazrui amesema mkutano huo umeonyesha namna wanavyoweza kushirikiana na kupata mbinu tofauti za kushughulikia changamoto za afya

Ametumia fursa hiyo kuwataka wataalamu hao kufanya tafiti mbalimbali za afya kwani zimeonyesha zinavyoleta mabadiliko chanya na kupata ufumbuzi wa changamoto.

Kongamano hilo la 11, limefanyika kwa siku tatu na kuwashirikisha wataalamu kutoka ndani na nje ya nchi lengo ni kujadili na kutafuta suluhisho la matatizo yanayoikumba sekta ya afya.

 

Visitor Counter

000833
Today: 3
Yesterday: 6
This Week: 41
Last Week: 60
This Month: 165

Opening Hours

  • Monday: 8.30am–6.30pm
  • Tuesday: 10.00am–8.00pm
  • Wednesday: 8.30am–6.30pm
  • Thursday: 8.30am–7.00pm
  • Friday: 8.30am–3.00pm
  • Saturday: 8.30am–2.00pm
  • Sunday: 8.30am–2.00pm

Contact Us

Kanani A Road, Mumasama Street,

P.O.BOX, 137

Ngara, Tanzania

Mobile:  +255 744 172 741

Email: info@ishizwemedia.co.tz